Mark 7:5-10

5 aKwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria wakamuuliza Isa, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee, na badala yake wanakula kwa mikono najisi?”

6 bIsa akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa: “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,
lakini mioyo yao iko mbali nami.

7 cHuniabudu bure,
nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’

8 dNinyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.”

9 eNaye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu! 10 fKwa mfano, Musa alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’
Copyright information for SwhKC